Mungu Mwenye Nguvu

Lyrics

Halleluya,
 Ndugu yangu Biblia inasema
 waabudio halisi watamwabudu Bwana
 katika roho na kwa kweli
 Na ni wakati huu – ukiwa ndani ya gari lako,
 ukiwa ndani ya basi unasafiri,
 ukiwa unafanya kazi ndani ya ofisi yako
 Jiunge pamoja nami tumwinue Bwana
 tumwambie wastahili uko mwenye nguvu
 Ukiwa uliamka asubuhi
 na haukumwambia kitu Mungu,
 ni wakati wa kumwambia Bwana:
 Utukuzwe, uinuliwe
 Tujiunge pamoja kwa wakati huu
 tumwambie Bwana "Wastahili"
 Ikiwa uko katika maombi ya kufunga na kuomba,
 hebu tujiunge pamoja, Twende Haleluya
 Mungu wetu mwenye nguvu, ni Baba wa Milele
 (Mungu wetu mwenye nguvu, Baba wa milele)
 Eeh Eeh Ni Mwenye nguvu, Ebeneza Baba wa milele
 (Mungu wetu mwenye nguvu, Baba wa milele)
 Wanipa mema, wewe ni mwenye nguvu, Baba wa milele yote
 (Mungu wetu mwenye nguvu, Baba wa milele)
 Nguvu zako zashangaza Dunia, uliumba mbigu pasipo nguzo,
 hewani Baba.
 (Mungu wetu mwenye nguvu, Baba wa milele)
 Uko mwema, Bwana, matendo yako ni ya ajabu sana aaaaa
 Neema yako, fadhili zako, kila asubuhi
 Ni mpya tena zanifariji moyo niamkapo baba
 Nikikosewa na maisha, wanipa tumaini la kupata maisha Baba
 Wajapo nicheka majirani wangu
 Wewe upo upande wangu, Uhimidiwe Yahweh
 Neema yako, fadhili zako, kila asubuhi
 Ni mpya tena zanifariji moyo niamkapo
 Wanipa tumaini la maisha Baba yangu o duniani
 Natembea nawe Baba yangu,
 Hujaniacha mimi o Baba
 Neema yako, fadhili zako, kila asubuhi
 Ni mpya tena zanifariji moyo niamkapo
 Wanipa tumaini la maisha Baba yangu oooh duniani
 Natembea nawe Baba yangu,
 Hujaniacha mimi
 oooh Baba.
 Neema yako, fadhili zako, kila asubuhi
 Ni mpya tena zanifariji moyo niamkapo
 Kulala, kuamka
 ni kwa neema yake Mungu, Ndugu yangu,
 Ulimpa mungu nini wewe
 kusudi uwe jinsi ulivyo?
 Usijivune bure ni neema yake baba.
 Neema yako, fadhili zako, kila asubuhi
 Ni mpya tena zanifariji moyo niamkapo
 Aiiiii, Yesu, nani kama wewe Bwana, Sina mwingine kukuliko wewe, mfalme wa dunia ni wewe, mwanzo na mwisho ni wewe Baba aaa oh Yesu
 Baba utukuzwe, Baba uinuliwe
 Rafiki yangu, I love you, I love you, I love you Baba yo
 Baba utukuzwe, Baba uinuliwe
 Maneno yako yafungua watu, yafungua watu, yafungua watu
 Baba utukuzwe, Baba uinuliwe
 Sitasahau uliponitoa, Umenitoa mbali, umenitoa mbaali baba
 Baba utukuzwe, Baba uinuliwe
 Oooh oooh, uhimidiwe yahweh
 Baba utukuzwe, Baba uinuliwe
 Rafiki yangu nakupenda sana, nakupenda sana, nakupenda sana Baba eeh
 Baba utukuzwe, Baba uinuliwe
 Rafiki yangu I love you, I love you, I love you, I love you
 Baba utukuzwe, Baba uinuliwe
 Sitasahau ulikonitoa, Umenitoa mbali, umenitoa mbaali baba
 Baba utukuzwe, Baba uinuliwe
 Maneno yako Yana nguvu sana, Yana nguvu sana, Yana nguvu sana Baba
 Baba utukuzwe, Baba uinuliwe
 Kwa neno lako Lazaro kafufuka, kafufuka, Kafufuka Yesu wangu
 Baba utukuzwe, Baba uinuliwe
 Rafiki yangu nakupenda sana, nakupenda sana, nakupenda sana Baba
 Baba utukuzwe, Baba uinuliwe
 Oooh oooh, Baba, ooooo, Baba, ooooo Baba, mmmmmm, noono, ooooo,, Baba yoyyo

Audio Features

Song Details

Duration
07:32
Key
4
Tempo
144 BPM

Share

More Songs by Solomon Mukubwa

Similar Songs