Ameniona

2 views

Lyrics

Mmmmm ye ameniona huyu Yesu ee
 Hallelujah mmmmm.
 Mimi nilikuwa kipofu muda wa siku nyingi
 Sikupata msaada kwa mwanadamu yeyote
 Yesu alipokuja kapaka udongo machoni mwangu
 Sasa nimeona acha nishuhudie makuu yake hallelujah
 Ooooo Yesu ameniona
 Ooooo Yesu ameniona
 Mimi nilitokwa na damu miaka kumi na miwili
 Waganga na madaktari hawakuweza kuniponya
 Nilipomuona Yesu nikagusa pindo la nguo yake
 Damu ikakauka sasa mimi nimepona hallelujah
 Ooooo Yesu ameniona
 Ooooo Yesu ameniona ×2
 Nilitoza kodi miaka mingi iliyopita
 Niliwaibia watu wengi waliteseka kwa ajili yangu
 Nikapanda juu ya mti Bwana Yesu akaniona akanisamehe nikalipa madeni yote hallelujah
 Ooooo Yesu ameniona
 Ooooo Yesu ameniona ×2
 Ameeeeeeniona ameniona Yesu wangu
 Ninapo-omba mimi ninapo-lia mimi
 Nipitapo chini ya bonde la uvuli wa mauti
 Yesu wangu ameniona
 Hallelujah
 

Audio Features

Song Details

Duration
04:20
Key
7
Tempo
73 BPM

Share

More Songs by Angela Chibalonza

Similar Songs