Dunia Ina Mambo

2 views

Lyrics

Shetani akamwuliza Mtakatifu Petero
 Umewahi kuangalia huko chini (aye aye)
 Mtu maskini akiiba mkate
 Atavalishwa pingu miaka minne (aye aye)
 Lakini tajiri anayezorotesha
 umaskini wa nchi nzima (mwajijua)
 Anachekacheka na hakimu
 Baadaye wapo wote pamoja mikahawani
 Dunia ina mambo
 Kweli ina mambo
 Dunia ina mambo
 Dunia ina mambo
 Nyuma ya kila mlango
 Dunia ina mambo
 Shetani akamwuliza Mtakatifu Petero
 Ni dini gani inayoendeleza chuki (mambo bado)
 Kwa ajili ya bidii ya bin adam
 Mimi sina kazi (mambo bado)
 Warumi wachukia wakristo wengine
 Wengine wachukia Waislamu (bure bilash)
 Waislamu wachukia Wayahudi
 Na nguvu zangu zote singeweza hayo yote
 Dunia ina mambo
 Kweli ina mambo
 Dunia ina mambo
 Dunia ina mambo
 Vituko na vichekesho
 Dunia ina mambo
 Shetani akamwuliza Mtakatifu Petero
 Ni kulala mnalala au vipi (hallo hallo)
 Mnaruhusu viongozi wa nchi tajiri
 Kumiliki nchi masikini (hallo hallo)
 Kwa mfano wananchi wa nchi zilizokuwa chini ya ukoloni
 Waliporwa mali zao au siyo (au siyo)
 Basi mbona walionyanyaswa wasipande ndege
 Na kwenda ng'ambo ili kurudisha haki zao
 Dunia ina mambo
 Kweli ina mambo
 Dunia ina mambo
 Dunia ina mambo
 Mbele ya kila wazo
 Dunia ina mambo
 Dunia ina mambo
 Kweli ina mambo
 Dunia ina mambo
 Dunia ina mambo
 Mbele ya kila wazo
 Dunia ina mambo
 Dunia ina mambo
 Kweli ina mambo
 Dunia ina mambo
 Dunia ina mambo
 Vituko na vichekesho
 Dunia ina mambo

Audio Features

Song Details

Duration
04:09
Key
2
Tempo
105 BPM

Share

More Songs by Eric Wainaina

Similar Songs