Nchi Ya Kitu Kidogo

3 views

Lyrics

Mzee alisema hakuna cha bure
 huo msemo tunautafsiri kinyume ee
 hata shule kuingiza mtoto
 lazima utoe mchoto
 kupata simu ni balaa
 Road license bei nafuu 'tanunua
 kupoteza ID ni mashaka, twarudisha jamhuri yetu nyuma
 Nchi ya kitu kidogo, ni nchi ya watu wadogo
 ukitaka chai ewe ndugu, nenda Limuru(nenda Limuru)
 Hata nyumbani ukipatwa na majambazi, kupigana naye wasema sisis hatuna gari
 lete elfu tano ya petroli, saidia utumishi
 Mahakamani hela ndio haki
 kwa elfu chache mshtakiwa ndiye mshtaki,
 utajiri huwa ushahidi
 twarudisha jamhuri yetu nyuma
 nchi ya kitu kidogo
 ni nchi ya watu wadogo
 ukitaka soda ewe inspekta, burudika na Fanta
 nchi ya kitu kidogo
 ni nchi ya watu wadogo
 ukitaka chai ewe mama, nunua ketepa
 (aha)
 Huko Kenyatta madawa zimeisha
 masheet zauzwa marikiti mia kwa mia
 wafanyikazi waenda miezi bila pesa
 ni bahati ukitibiwa
 mzigo wetu unazidi kuwa mzito
 watoto wanne na mshahara wa elfu mbili
 mia tano ya vitabu viatu na vyakula, nauliza na Mbotela vje huu ni uungwana'
 nchi ya kitu kidogo
 ni nchi ya watu wadogo
 ukitaka chai ewe ndugu nenda limuru
 nchi ya kitu kidogo
 ni nchi ya watu wadogo
 ukitaka chai ewe mama, nunua Ketepa(nunua Ketepa)

Audio Features

Song Details

Duration
04:38
Key
8
Tempo
123 BPM

Share

More Songs by Eric Wainaina

Similar Songs