Naiona Kesho

3 views

Lyrics

Naiona kesho kesho
 Iliyopangwa na baba
 Naiona kesho kesho
 Iliyopangwa na mungu
 Naiona kesho mimi kesho iliyopangwa na baba
 Kesho ya heshima aah
 Iliyopangwa na baba kesho ya Neema iliyopangwa na baba
 Kesho yenye utukufu iliyopangwa na
 baba kesho ya kuinuliwa iliyopangwa na baba
 Kesho ya ushindi ii iliyopangwa na mungu
 Kesho yenye nguvu iliyopangwa na baba
 ♪
 Sitaki kuitazama Leo yangu mwenzenu
 ♪
 Leo yangu ni shida. Mwenzenu
 Leo yangu ni tabu mwenzenu
 Leo machozi yanitoka aah mwenzenu
 Leo nimekataliwa aah mwenzenu
 Leo nimefukuzwa mapema mwenzenu
 Leo wote waniacha aah mwenzenu
 Leo machozi ni mengi hii mwenzenu
 Sitaki kuitazama Leo yangu kamwe
 Sitaki kuitazama Leo yangu mm
 Leo yangu ninalia mwenzenu
 Leo ninateseka aah mwenzenu
 Leo mateso ni mengi hii mwenzenu
 ♪
 Naiona kesho yangu mwenzenu x 2
 ♪
 Japo vita yangu ni kubwa mwenzenu
 Maadui wangu ni wengi mwenzenu
 Japo mateso yangu ni magumu mwenzenu
 Kuna neno amesema nami mwenzenu
 Atapigana aah amesema
 Atafanya mlango ooh amesema
 Atanifanyia wepesi amesema
 Japo vita yangu kubwa mwenzenu
 Japo adui ni wengi mwenzenu
 Japo njia siioni mwenzenu
 Atapigana mwenyewe amesema
 Atafanya wepesi iiih amesema
 Atanifanyia wepesi kwani amesema
 Atanichunga salama mh amesema
 Atafanya mlango ooh amesema
 Atapigana na adui aah amesema
 Kasema niione kesho aliyoniwekea ×2
 ♪
 Kuna majira yalifika nikajua mungu
 Kuna majira yalifika nikamwelewa
 Majira Yale yalikuwa magumu ×2
 Kwa macho yangu nikaona akitenda ×2
 Akasema mwanangu nakupenda ×2
 Usiitazame Leo yako mwanangu ×2
 mbona mimi ni mungu nikupendaye ×2
 Ni kweli kwa macho ya nyama Mimi nimechoka wengi wanitazamapo kweli
 ♪
 Nimeshindwa
 Wengi wanionavyo kweli nimeshindwa
 Kweli kwa mbio za Mimi nimechoka
 Kweli kwa mwendo wangu nimeshindwa
 Kwa macho ya nyama nimechoka
 Kwa macho ya watu nimeshindwa
 Lakini hakuna hata mmoja. Anayejua
 Patano langu na mungu
 Lakini hakuna hata mmoja anayejua nimepatana nini
 Tumepatana na Baba hataniacha
 Hata nikisukwa sukwa sitamuacha
 Hata nikilia nisimuache
 Hata nikiteseka aah nisimwache
 Tumepatana na baba
 Nimepatana na baba × 3
 Naiona kesho yangu iliyonjema haa
 Naiona kesho iliyonjema haa . Mwenzenu Naionaaaa kesho
 Naiona kesho kesho iliyopangwa na baba(kesho ya heshima)
 Naiona kesho kesho iliyopangwa na mungu (kesho ya Neema)
 Naiona kesho kesho iliyopangwa na baba(kesho ya kufanikiwa)
 Kesho ya heshima aah, kesho ya utukufu iliyopangwa na baba
 Kesho ya heshima (ya heshima yangu na Mimi)
 iliyopangwa na mungu (kesho ya wote kumjua mungu wanguuu)
 ♪
 Kesho ya heshima iliyopangwa na baba
 ♪
 Kesho ya ushindi iliyopangwa na mungu
 Kesho ya utukufu wangu iliyopangwa na baba
 Kesho × 3
 

Audio Features

Song Details

Duration
09:15
Key
2
Tempo
178 BPM

Share

More Songs by Martha Mwaipaja

Similar Songs