Nikumbushe Wema Wako

3 views

Lyrics

Nirahisi kinywa kujawa na lawama tele
 pale mambo yanapoonekana hayaendiii
 ni ajabu sana namna moyo unahangaika (kutafuta majibu)
 Ajabu sana moyo unavyoonyesha mashaka yakwamba japokuwa Mungu anaishi ndani yangu kuna muda nahofu, japokua Mungu anaketi kati yetu kuna muda nahofu,
 ahh nakumbuka wana wa Israel katika bahari yashamu japo walikatiza katikati ya bahari kwa ushindi,
 kwa nyimbo nyingi waliimba na kumsifu Bwanaa. Lakini baada ya kuvuka na kuliona jagwa yalibadilika mambo,
 manung'unikoo yalisimama na kusahau muujiza alotenda Bwana Mwanzo aah.
 Eee MUNGU Niisaidieee eee eenhee
 BRIDGE -Nikumbushe wema wako nisije laumu
 Nikumbushe ukuu wako wakati wa Magumu
 Nikumbushe shuhuda zako ili nikusifu
 niimbe wimbo wa sifa katikati ya machoziii, x2
 Eeeh Ee MUNGU Nisaidiee
 Nisaidieee kukumbuka baba yakwamba umenichora kiganjani mwako kati ya wengi walioko duniani eenh na mimi umenionaa oooh ooo
 Nikumbushe baba yakwamba ni wewe umeniponya nilipoumwa yakwamba ni wewe mlipaji wa ada yangu shuleniii. ouoooh ooh
 Yakwamba kama ungeniacha hatua moja nisingelifika nilipo ooh eee Babaa umenikung'uta mavumbi, kung'uta mavumbi mimi na kuniheshimisha.
 oooooh oooooh
 Nikumbushe wema wako nisije laumu
 Nikumbushe ukuu wako wakati wa Magumu(Nisaidie Yesu)
 Nikumbushe shuhuda zako ili nikusifu
 niimbe wimbo wa sifa katikati ya machozii ×2

Audio Features

Song Details

Duration
07:19
Key
6
Tempo
111 BPM

Share

More Songs by Angel Benard

Similar Songs