Nakupenda

3 views

Lyrics

Bwana Yesu nakupenda, wewe uliyenipenda mimi
 Sina chochote cha kulipa chalingana na upendo wako
 Ya thamani yote ni yako
 Ata hivyo yasingeweza kulipa
 Uliotenda ni makuu sana mimi siwezi kueleza
 Yanishangaza, yanipita je niseme nini, bwana wangu
 Mwanadamu nisiyestahili
 Kunipenda ata kunifia, eh bwana
 Bwana wetu, eeh Mungu wetu
 Twasimama mbele zako bwana
 Tumekujaa kukushukuru bwana
 Na kukusifu usifiwe milele (ewe bwana)
 Bwana wetu, eeh Mungu wetu
 Twasimama mbele zako bwana (tumekujaa)
 Tumekujaa kukushukuru bwana (na kukusifu)
 Na kukusifu usifiwe milele (ewe bwana)
 Ungeweza kutojali mwanadamu akaangamia
 Kwa kuwa yeye ndiye aliitenda dhambi sio wewe bwana
 Ungeweza kumuumba mwengine
 Mwenye dhambi, usimkumbuke tena
 Lakini kinachoshangaza maamuzi yako ni kinyume
 Uliamua kumpenda yule-yule ambaye apendeki
 Eeh bwana tuseme nini
 Pendo lako limetuzidi, eh bwana
 Bwana wetu, eeh Mungu wetu
 Twasimama mbele zako bwana (tumekujaa)
 Tumekujaa kukushukuru bwana
 Na kukusifu usifiwe milele (ewe bwana)
 Bwana wetu, eeh Mungu wetu
 Twasimama mbele zako bwana (tumekujaa)
 Tumekujaa kukushukuru bwana
 Na kukusifu usifiwe milele
 ♪
 Ndugu yangu fikiria sana pendo hili la thamani
 Tutapata je kupona tusipolijali pendo hilo
 Kila jambo limewekwa wazi
 Karibia msalaba wake
 Ebu njooni twende kwake tuzitubu dhambi zetu zote
 Hatuna muda tena ndugu, pendo hili lisipite bure
 Ni salama mikononi mwake
 Mtetezi tena ushindi wetu (eh bwana)
 Bwana wetu, eeh Mungu wetu
 Twasimama mbele zako bwana (tumekujaa)
 Tumekujaa kukushukuru bwana (na kukusifu)
 Na kukusifu usifiwe milele (eh bwana, eh bwana, eh bwana)
 Bwana wetu, eeh Mungu wetu
 Twasimama mbele zako bwana (tumekujaa)
 Tumekujaa kukushukuru bwana (na kukusifu)
 Na kukusifu usifiwe milele (ewe bwana)
 Bwana wetu, eeh Mungu wetu (ewe bwana)
 Twasimama mbele zako bwana (tumekujaa)
 Tumekujaa kukushukuru bwana (na kukusifu)
 Na kukusifu usifiwe milele
 

Audio Features

Song Details

Duration
05:10
Key
3
Tempo
98 BPM

Share

More Songs by Ambassadors Of Christ Choir

Similar Songs